Idadi
ya waliofariki dunia kutokana na Kimbunga kikubwa cha Sandy huko nchini
Marekani imefikia 16 ambapo zaidi ya nusu ya vifo hivyo vimetokana na
watu hao kuangukiwa na miti.
IDADI ya waliofariki dunia kutokana na Kimbunga kikubwa cha Sandy
huko nchini Marekani imefikia 16 ambapo zaidi ya nusu ya vifo hivyo
vimetokana na watu hao kuangukiwa na miti.
Vifo hivyo kwa ujumla wake vimeripotiwa katika majimbo ya New York,
New Jersey, West Virginia, Connecticut, Pennsylvania na Maryland. Lakini
kuna vifo vingine pia vimeripotiwa kutokana na kukatika kwa umeme na
ajali ya gari katika balaa la kimbunga hicho.
Kuna ripoti ya mwanamke mwingine kufariki dunia kutokana na kimbunga
hicho na mwili wake kuonekana ukielea katika maeneo ya bahari,huko
Toronto nchini Canada jumapili. Kwa mujibu wa kituo cha televisheni cha
CNN Kimbunga hicho mpaka sasa kimeacha zaidi ya raia milioni 6.5 nchini
Marekani pasipo nishati ya umeme katika eneo la Pwani ya Mashariki.
New York yaathirika zaidi
Vehicles are submerged on 14th Street near the Consolidated Edison power
plant, Monday, Oct. 29, 2012, in New York. Sandy continued on its path
Monday, as the storm forced the shutdown of mass transit, schools and
financial markets, sending coastal residents fleeing, and threatening a
dangerous mix of high winds and soaking rain. (AP Photo/ John
Minchillo) Jiji la New York
New York ni miongoni mwa mji ulivurugwa vibaya na kimbunga hicho
ambacho rekodi zinaonesha kiliambatana na mawimbi ya urefu wa meta 4
katika eneo la kusini la Manhattan. Katika eneo hilo maji yalifurika
mpaka katika njia kubwa kabisa ya reli. Na soko la hisa la New York
limeendelea kufungwa kwa siku ya pili mfululizo.
Duru nyingine zinaeleza kwamba moto uliowaka usiku kucha umeteketeza
takribani nyumba 50 katika kitongoji cha Queens. Taarifa hizo
zimesambazwa na kitengo cha zimamoto kupitia ukurasa wake wa Twiter
ambapo hata hivyo hakikutoa maelezo zaidi kufuatia mkasa huo. Lakini
kama inavyofahamika kwamba mkasa huo umetokea baada ya kimbunga Sandy
kuyakumba maeneo ya Pwani ya Mashariki ya Marekani ukiwemo mji wa New
York.
Hata hivyo balaa la kimbunga hicho bado halijafika kikomo ambako
wasiwasi bado upo katika maeneo ya mbali ya majimbo ya Wisconsin na
Ilinois. Ishara ya tahadhari imetolewa kuanzia Chicago mpaka Maine na
Canada mpaka Florida. Tahadhari hiyo inaonesha kimbunga Sandy
kitaendelea kuwa tatizo katika siku kadhaa zijazo na kitaambatana na
mvua kali, theluji na mafuriko. Wakaazi walio katika eneo la Michigan na
Ontario wametahadharishwa kuwepo kwa mawimbi makubwa. Na pia theluji
zaidi kama ilivyo katika baadhi ya maeneo ya Atlantik ya kati.
Hali hiyo imezorotesha kampeni za uchaguzi wa rais wa Marekani ambapo
Rais Barack Obama na mpinzani wake Mitt Romney wanafuatilia kazi ya
uokozi katika maeneo ya yalikumbwa na kimbunga hicho.
-DW
0 Comments