MAANDALIZI YA HARUSI YAKAMILIKA

MAANDALIZI YA HARUSI YAKAMILIKA


Harusi kati ya Bw. Shuma/Saashisha Elinikyo Mafuwe na Bi. Oliver Lufingo Msalilwa yameanza kukamilika, Harusi hiyo itakayofungwa katika Kanisa la Azania Front - Kivukoni Jijini Dar es Salaam siku ya tarehe 1 Septemba' 2012 na kisha tafrija yake ya kukata kwa mundu itafanikishwa katika ukumbi maridhawa na maarufu wa Msimbazi Centre (Maranta Hall) Ilala Jijini Dar es Salaam.


 

BW. SHUMA MAFUWE NA BI. OLIVER MSALILWA


BW. SHUMA MAFUWE NA BI. OLIVER MSALILWA KATIKA POZI BEACH



WAPENDANAO BW. SHUMA MAFUWE NA BI. OLIVER MSALILWA

 Akiongea na Makamu Mwenyekiti Mr. Grayson Msafiri Mwikola na Katibu wa Sherehe hiyo Mr. Godfrey Peter Minguzi, kwamba kila kitu kimekamilika na maandalizi ni ya kufa mtu. wageni waalikwa watakunywa, watacheza na hali ya usalama wao binafsi ni ya hali ya juu.


Erick Athanas Urio - Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi

Makamu Mwenyekiti Bw. Grayson Mwikola kushoto na Katibu Bw. Godfrey Peter Minguzi

 

Katibu wa Kamati ya Maandalizi Bw. Godfrey Peter Minguzi

  Makamu M/Kiti wa Kamati ya Maandalizi Bw. Grayson Msafiri Mwikola



             Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi Bw. Erick Athanas Urio

Kamati hii adhimu inaongozwa na Mwenyekiti Mahiri na mzoefu wa kusimamia ndoa za vijana ili waishi milele katika ndoa yao na Bw. Ephraim Semu Mafuwe akisaidiwa na Makamu M/Kiti Bw. Grayson Mwikola, kwa upande wa Uratibu wa shughuli zote za Kamati yupo Bw. Godfrey Peter Minguzi. Huku nafasi ya Mtunza ATM akiwa ni Bi. Carlorine Stewart Swai. Kama hiyo haitoshi basi siku ya siku usimamizi mzima za shughuli za Sherehe ukumbini zitasimamiwa barabara na Bw. Ephraim Semu Mafuwe.

 

Kamati ikaona ni bora kuwatafuta watenda kazi waliobobea na kazi zao (professionals) katika fani mbalimbali kama ifuatavyo:- Mapambo yupo mpambaji mwenye tunzo kibao Grayson Mwikola (Grayson Decorations). Chakula yupo Mama mzoefu na shughuli hizi, chakula kitamu na kisichoisha hamu huyu ni Mama Mahindi na (Mahindi Catering Services), Keki yupo anayepikia mabalozi mbalimbali Mr. Frank Mafuwe.

 

Upande wa Mshereheshaji si mwingine ni MC MAKAME anayekwenda na muda na matukio ya kubamba. Sambamba na ma-DJ wajanja wanaokwenda na time.

 

Kumbukumbu za picha za still yupo kijana mbunifu na mahiri kwa shughuli hizi: Mr. Matiku  na (Matiku Photo Expo 2012). Bila kumsahau Video Operator mwenye professional zake kibao Hassan Haji Ndunda toka HVP Studio (The digital artist video professional), "Asili na Halisi Haipotei" Kigamboni Dar es Salaam.

 

Sherehe hii itarushwa live kwa projector tatu ukumbini. 

 

Ahsanteni Sana,

 

Post a Comment

0 Comments